Mark 10:32-34

32 aWalikuwa njiani wakipanda kwenda Yerusalemu, na Isa alikuwa ametangulia. Wanafunzi wake walishangaa, nao watu waliowafuata walijawa na hofu. Isa akawachukua tena wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia yatakayompata. 33 bAkasema, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atasalitiwa kwa viongozi wa makuhani na walimu wa sheria. Wao watamhukumu kifo na kumtia mikononi mwa watu wa Mataifa, 34 cambao watamdhihaki na kumtemea mate, watampiga na kumuua. Siku tatu baadaye atafufuka.”

Ombi La Yakobo Na Yohana

(Mathayo 20:20-28)

Copyright information for SwhKC